Askari Usalama Barabarani atiwa mbaroni kwa Rushwa ya Sh.5,000 Unguja

Mamlaka yakuzuia Rushwa na uhujumu uchumi Zanzibar(ZAECA ) imemtia mikononi Askari Polisi wa usalama Barabarani kwatuhuma ya kuomba rushwa ya shilingi 5,000.

Kwamujibu wa taarifa kutoka kwa Afisa wa uhusiano Mamlaka ya kuzuia Rushwa na uhujumu Uchumi Zanzibar Mwanaidi Suleiman ameeleza kuwa kituo cha Polisi Mazizini Mkoa wa Mjini Magharib Unguja kimemshikilia Koplo ambae ni mtumishi wa Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kituo cha mazizini kwakuomba rushwa  ya sh.5,000 kwa dereva wa daladala za abiria ambaye jina lake limehifadhiwa.

Afisa huyo ameendelea kueleza kuwa Dereva wa gari hiyo tayari alikua ameshaonesha Vielelezo vyake vya usajili wa barabarani lakini Askari huyo ameendelea kulazimisha makosa nakumtaka ampe sh.5,000 ndipo ambapo Dereva wa gari hiyo kuelekea mamlaka yakuzuia Rushwa (ZAECA) kutoa taarifa.

Afisa Mwanaidi ametoa wito kwa watumishi wa umma kuwa wafanye kazi kwamujibu wa taratibu zilizopangwa pamoja na kuwaomba wananchi kutofumbia macho vitendo kamaivo kwa lengo la kukomeshwa kwa watendaji wa matukio kama hayo ili kuleta maendeleo ndani ya nchi.