Klopp aanza kuchonga Liverpool

Jurgen Klopp amesema ana kikosi kizuri kinachoweza kuifunga timu yoyote duniani kwa sasa baada ya kuichapa Manchester City kwa mabao 2-1 ugenini kwenye Uwanja wa Etihad na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa magoli 5-1.

Mohamed Salah alifunga bao lake la 39, msimu huu akiwa na jezi ya Liverpool, pia Misri huyo alitegeneza bao la pili lililofungwa na Roberto Firmino na kukujihakikishia ushindi mnono wa mabao 2-1 ugenini.

Pep Guardiola alicheza kamari katika mchezo huo wa marudiano kwa kuwaanzisha washambuliaji saba, na kufanikiwa kupata bao la mapema dakika 11 lililofungwa na Gabriel Jesus, lakini mambo yalibadilika kipindi cha pili katika dakika 11 za mwisho.

Kauli hiyo ya kocha huyo wa Liverpool imekuja muda mfupi baada timu  hiyo kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya juzi usiku.

 “Nadhani nina kikosi bora cha aina yake ambacho kinaweza kufunga timu yoyote duniani. Tulijua tutashinda na kusonga mbele katika mchezo wa marudiano,” alisema Klopp.

Kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund alisema kipigo hicho kimemvunja nguvu Pep Guardiola.

Klopp alisema ana furaha baada ya kuivusha timu hiyo kucheza nusu fainali na mkakati wake ni kuanza maandalizi mapema.

Kocha huyo Mjerumani alisema dunia imetulia baada ya ushindi wa Liverpool.