Dogo Janja ampagawisha uwoya hadi atoa zawadi

Ndoa kati ya muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya na staa wa muziki wa Bongofleva Dogo Janja inaonekana yazidi kupamba moto baada ya wawili hao kuamua kuweka mapenzi yao hadharani na kutokujali wa wanaowakosoa kwa kupishana kwao umri.

Irene Uwoya azidi kuonyesha mapenzi kwa mume wake Dogo Janja baada ya kuamua kuchora tattoo katika mwili wake nakuandika Abdul ambalo ni jina halisi la mume wake Dogo Janja.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dogo Janja, amepost picha ya mkewe inayoonyesha Tattoo hiyo na kumuandikia maneno yafuatayo:-

Ahsante Mke Wangu, Nichore Na kule Ninapopaonaga mimi tu