Raia wa Denmark akutwa hana hatia ya mauaji ya Mama na mwanae

Mume wa msanii wa Nigeria Alizee ambaye ni raia wa Denmark Bw. Peter Nielsen, amekutwa hana hatia kwenye kesi ya mauji ya msanii huyo sambamba na mtoto wao wa kike, yaliyotokea wiki iliyopita.

Kesi hiyo ambayo ilifunguliwa wiki iliyopita baada ya tukio la mauaji ya msanii huyo na mtoto wake wa kike wa miaka minne, lililotokea nyumbani kwake katika eneo la Banana nchini Nigeria, huku mume wake kuwa mshukiwa wa kwanza baada ya kukutwa alama za vidole vyake kwenye mwili wa marehemu.

Hata hivyo mahakama ya Nigeria haijaelezea ni kwa namna gani mtuhumiwa huyo amekutwa hana hatia, na kesi hiyo imehairishwa mpaka tarehe 8 Juni, 2018.

Baba wa msanii huyo Ali Madaki aliwahi kunukuliwa akisema kwamba mwanaume huyo alikuwa na tabia ya kumpiga sana binti yake, na mara nyingi alikuwa akienda kumshtakia.

Alizee ambaye jina lake halisi ni Zainab Ali, ameuawa Aprili 5, 2018, na mwili wake kutelekezwa jikoni chini ya gesi sambamba na mwili wa mtoto wake, ikielezwa kwamba lengo likiwa ni kufanya ionekane wamekufa kwa kuvuta gesi hiyo.