Vikao vya EALA kufanyika katika kumbi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kwa mara ya kwanza vikao vya Bunge la Afrika Mashariki, (EALA) vitafanyika Dodoma katika moja ya kumbi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Spika ameyasema hayo leo Aprili 12, mara baada ya kuwatambulisha wabunge kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki walioshiriki  katika kikao cha bunge leo.

Spika Ndugai aliwatambulisha wabunge kutoka nchi za Sudan Kusini, Rwanda, Kenya, Burundi na Uganda na kuwataka wabunge wa Tanzania kushirikiana nao na kujifunza kutoka kwao.

“Tuna matumaini makubwa kupitia kwenu, wabunge wetu wanaangalia mnafanyaje mambo yenu huko. Kwa pamoja tutahakikisha shughuli zinakwenda vizuri.” Amesema