Wito wizara ya fedha na mipango – Pemba

Tume ya Utumishi Serikalini inawatangazia wale wote walioomba nafasi za kazi Wizara ya Fedha na Mipango – Pemba na ambao walifanya usaili wa awali tarehe 26/03/2018 kwamba wafike Skuli ya Fidel Kasro – Pemba kwa ajili ya kufanya usaili wa mara ya Pili kwa utaratibu ufuatao hapo chini:-

Wasailiwa wote wanatakiwa wachukue vyeti vyao halisi vya kumalizia masomo, Cheti cha kuzaliwa pamoja na kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.

MCHANGANUO WA USAILI WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO PEMBA

NAM. TAREHE NAFASI YA KAZI

1. 14/4/2018 MKAGUZI WA NDANI DARAJA LAII

2. 15/4/2018 MHASIBU DARAJA LA II

3. 16/4/2018 MSAIDIZI MHASIBU DARAJA LAIII

KARANI MAPATO DARAJA LA III

4. 17/4/2018 MHAKIKIMALI DARAJA LA II

5. 18/4/2018 MHAKIKIMALI MSAIDIZI DARAJA LA III

AFISA UTUMISHI MSAIDIZI DARAJA LA III

Mahala pa usaili wote huo utafanyika katika Skuli ya FIDEL KASRO PEMBA.