Aliyo ya sema Vanessa mdee baada ya Jux kusaini dili nchini China

Kufuatia tukio lilotokea jana, April 12, 2018 ambapo Jux kupitia brand yake ya African Boy alisaini dili nchini China. Sasa mpenzi wake, Vanessa Mdee hajawa nyuma kwenye hilo.

Vanessa Mdee amempongeza Jux kwa hatua hiyo aliyopiga na kuwashukuru watu wote waliokuwa waki-support bidhaa za Jux kupitia African Boy. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Vanessa ameandika:-

We live in a world of endless possibilities. Hongera sana sana sana babe, umepambana sana kuijenga African Boy pamoja na Watanzania wote waliowahi ku-support brand yako ya kijanja, now it’s Money Time. God bless you with more Jux, nakuona mbali babi wewe piga kazi

Jux amesaini dili na kampuni  ya Vendome ya nchini China kwa ajili ya kuzalisha bidhaa zake kupitia brand ya African Boy ambayo ina bidhaa kama tisheti, kofia, viatu, mabegi n.k.