Halima Mdee, Ester Bulaya wawasili kituo cha Polisi

Mwenyekiti wa BAWACHA na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Ester Bulaya (MB) leo Ijumaa, April 13  wamewasili katika Kituo cha Polisi Kati jijini Dar es salaam .

Hatua ya Wabunge hao kuwasili kituo cha Polisi ni moja ya sharti la dhamana ambapo waliambiwa waripoti.

Viongozi Sita wa CHADEMA akiwemo Halima Mdee waliachiwa huru April 3 baada ya kutimiza masharti ya dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.