Mashindano ya kimataifa ya resi za baskeli kufanyika kesho zanzibar

Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale imeandaa Mashindano ya resi za Baskeli kwa lengo la kuutanganza Utalii Visiwani Zanzibar.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ikuhusiana na matayarisho hayo  katibu mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Dk  Vuai Iddi  amesema mashindano hayo yatajumuisha waendesha baskeli vijana kutoka nchi mbali mbali za Afrika, hivyo amewata wananchi kujitokeza kushangilia pamoja na kujionea uhondo wa mashindano hayo.

Amesea mashindano hayo yatasaidia kuongeza idadi ya Watalii nchini na kuongeza pato la taifa na  wananchi mmoja mmoja pamoja na ongeza la ajira kwa vijana.

Rais wa vijana wa Afrika Mashariki  Fest Peter George Mzunda amesema lengo la mashindano hayo ni kutangaza utalii pamoja na kuwapa fursa vijana kushiriki michezo ya baskeli na kuamsha hamasa kwa vijana kupata ajira kupitia mchezo huo.

Katibu mkuu wa Chama cha baskeli Zanzibar amesema kwa upande wa chama chao wameshukuru kupata nafasi ya kushiriki mchezo huo huku akisema wao wameweza kufanya mchujo na kuwapata wachezaji kumi kwa ajili ya mashindano hayo.

Akizungumza  kwa niaba ya mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,  Mkuu wa Trafiki wa Wilaya ya Mjini msaidizi wa Polisi Moh’d  Talhata  amesema kwa upande wa Jeshi la Polisi limejipanga kiusalama ilikuhakikisha mashindano hayo yanafanyika bila kuathiri shughuli za watu.

Mashindano hayo ya Afrika Mashariki na kati kwa kilomita 60 yanatarajiwa kuanzia uwanja wa Amani kupitia Mwera, Dunga, Jendele, Unguja Ukuu na kurejea kupitia barabara ya  Bungi, Fuoni, Mwanakwerekwe hadi uwanja wa Amani huku Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahamoud ambapo washiriki watatokea Tanzania bara, Kenya, Uganda, Burundi na wenyeji Zanzibar huku mataifa mengine yakialikwa katika Mashindano hayo wakiwemo Afrika ya Kusini, Zimbabwe, Zambia na Swaziland.