RC Makonda: Wanaume kuwapa mimba wafanyakazi wa ndani ni matokeo ya kutotumia kinga

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema, anayeona amefanya operesheni yake kwa kukurupuka ni mtenda dhambi.

Ameyasema hayo leo Aprili14, katika majohiano maalum yanayorushwa mubashara na televisheni ya TBC na kusema kuwa iwapo kesi zote za wenza hao zingepelekwa mahakamani, zingechukua muda mrefu.

Kadhalika amesema suala la wanaume kuwapa mimba wanawake nje ya ndoa au wafanyakazi wa ndani ni matokeo ya kutotumia kinga.

“Halafu wanataka niendelee kufanya mambo kwa maficho ili wao waendelee kuwapa watu ujauzito na kuwatelekeza,” amesema

Pia,  aliongeza: “Wale wote wangeenda mahakamani unafikiri ingechukua muda gani, pale kuna kesi zimesuluhishwa ndani ya muda mfupi na zimesha.”

Amesema mwanamke mnyonge hataweza kumudu gharama za mawakili kwa sababu ili asaidiwe ni lazima we na fedha.