Dogo Janja: Wasanii sisi ni masnichi sana aise

Rapa Dogo Janja amefunguka kuwa kwa sasa hana imani na wasanii wenzake wa muziki wa Bongo Fleva kwani wamekosa umoja na mshikamano hasa pale mmoja wao anapopatwa na tatizo.

Dogo Janja ametumia matukio mawili makubwa ambayo baadhi ya wasanii wa Muziki walishawahi kuyapitia yakiwemo ya kutekwa kwa Roma Mkatoliki na hili la juzi la video ya utupu ya Nandy na Bill Nass iliyovuja mtandaoni na kupata somo kuwa wasanii wengi wa muziki ni wanafiki na hawana umoja.

Kufuatia tukio la video chafu ya Nandy na Bill Nass, Mkali huyo wa Hip Hop amedai kuwa kuna baadhi ya wasanii wamefurahishwa na tukio hilo na wengine wakitaka BASATA wamfungie msanii huyo ili na wao wapate show.

Nahisi nnaweza kumaindiwa Leo na wasanii wenzangu ila lazima MTU aanze ndo hili donda ndugu litapona. Wasanii sisi ni masnichi sana aise, baada ya hii ishu ya nandy ndo nimepata uhakika. Wakati wa ishu ya Roma nilianza kuliona jinsi kwenye makundi pembeni watu kibao walikuwa wanafurahi tena maneno kibao kama atakoma, amezoea huyo…Jana na juzi nimekaa na watu wasanii wakubwa tu na wote walikuwa wanasema bora limemtokea nandy hili angalau spidi za show zitapungua…bora basata ingemfungia miezi 6 apotee kdg….walikuwa wanapiga story kama utani ila moyoni nimefikiria sana. Wasanii tuache roho mbaya, wote sisi maskini tunahangaikia ugali. Tukipata ajali kazini, tusiombeane mabaya tutafute amani…vita iwe kwenye kazi jamani. Hizi story za kufurahi ajali kazi mi nazikataa…

Ameandika Dogo Janja kwenye ukurasa wake wa Instagram.

A post shared by Dogo Janja (@dogojanjatz) on