Nandy ataja chanzo cha video yake na Bilnass kusambaa mitandaoni

Tangu jana mchana, gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii ni video ya mambo ya chumbani ya mwanamuziki Nandy na Bilnass iliyosambaa mtaani na kuzua taharuki kubwa katika tasnia ya sanaa nchini Tanzania.

Video hiyo ambayo kila aliyeiona alikuwa na jambo la kuzungumzia, inamuonesha mwanamuziki Nandy na Bilnass wakiwa chumbani huku wakishikana kwa mahaba, na hivyo watu wengi wakabaki wakijiuliza kwanini wasanii hao walisambaza video hiyo.

Licha ya kuwa kila shabiki alikuwa na upande wa kutupia lawama kuhusu kesi hiyo, wasanii wote wawili, Nandy na Bilnass wamesema kwamba hawahusiki na kusambaza video hiyo, lakini kwa upande wa Bilnass yeye amesema kwamba aamini mwenzie ndiye aliyeisambaza kwa lengo la kupata kiki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mwanamuziki Nandy ameandika waraka mrefu akielezea hali yake ilivyo kwa sasa na kwamba amepokea matusi kwa watu mbalimbali, lakini pia ameomba msamaha kwa watu wote kuhusiana na video hiyo.

“… naapa na naumia sana sana kwa hili lilitokea!!! sihusiki na kusambaza video wala siwezi ruhusu kitu kama hichi kitokee kwenye maisha yangu ya usanii hata ya kawaida!” ameandika Nandy.

Aidha, akijaribu kutafuta chanzo cha video hiyo kwenda mtandaoni, Nandy amesema kwamba huko nyuma amewahi kubadilisha simu mara mbili tangu 2016 lakini pia Bilnass amewahi kuibiwa simu yake, hivyo huenda kati ya matukio yake ya kubadilisha simu, au kuibwa kwa simu ya aliyekuwa mpenzi wake, ndiko kumepelea video hiyo kusambazwa mitandaoni.

“Naamini sababu kuu ya hii video kuwa out ni mambo ya simu zetu ambayo inaweza kumtokea mtu yoyote!! nilibadili simu yangu mara 2 toka 2016 na Bilnass aliibiwa simu yake huko nyuma, kwa mujibu wake, so hatujui mpaka sasa imetoka kwa simu ya nani?.

Nandy amekiri kwamba video hiyo aliirekodi yeye wakati akiwa kwenye uhusiano na Bilnass, lakini kwa namna yoyote ile asingewe kuruhusu video kama hiyo isambae mitandaoni.

“… sikatai nimerecord video na nilikuwa kwenye mahusiano na nilifanya kwa mapenz ila siwez weka public (hadharani).”

Mwanamuziki huyo amewashukuru wale wote waliopo nae katika kipindi hiki kigumu ikiwamo Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwani huu ni wakati mgumu sana kwake.

“… sante sana basata kwa ushirikiano wenu kwakuwa na mm na kunipa moyo hii ni fundisho kwa wote nimejifunza kitu kikubwa sana.”