Athari ya mvua Mwanakwerekwe Raia wahama na barabara kufunga Tazama Video+Picha

Mvua iliyonyesha kwa takribani siku 3 mfululizo imeanza kuonesha athari zake kufuatia maeneo mbalimbali ya mkoa wa mjini magharibi kufurika maji ikiwemo Mwanakwerekwe ambapo maji mengi yamefurika na kuvunja mawasiliano ya barabara ya mwanakwerekwe Fuoni.

Tazama video  maji mengi yamefurika na kuvunja mawasiliano ya barabara ya mwanakwerekwe Fuoni.

Aidha maji yalifurika na kusambaa hadi kwenye makaazi ya watu ambapo yaliingia majumbani mwa watu hali iliyopelekea baadhi ya familia kuacha makaazi yao katika maeneo ya karibu na ziwa la Mwanakwerekwe.

Tazama Picha maji yameingia katika makaazi ya watu.