RC Ayoub atoa rai kwa madereva wanaotumia barabara ya Fuoni kwa kipindi hiki cha mvua

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohd Mahmoud amewaagiza waendesha vyombo vya moto hususan gari za abiria wanapopita barabara ya Fuoni kutumia barabara mpya inayoanzia  Magogoni kutokea Kijitoupele ili kuepusha msongamano wa magari katika barabara ya nyumba mbili Kidarajani katika kipindi hichi cha mvua ambapo barabara kuelekea soko kuu Mwanakwerekwe haipitiki kutokana na maji ya ziwa la Mwanakwerekwe kufunga barabara hiyo.

Imetolewa na idara ya habari maelezo Zanzibar.