Donge imechafuka kwa madawa ya kulevya

Sheha wa Shehia  ya Donge Karange Saleh Khamis Ibrahim ameliomba jeshi la polisi kuzidisha  nguvu za doria katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika  kijiji cha donge kutokana na kijiji hicho kuongezeka kwa uuzwaji wa dawa za kulevya.

Akizungumza na Zanzibar24  amesema uuzwaji huo  wa madawa ya kulevya unaoendelea katika kijiji hicho usipodhibitiwa  unaweza kuleta athari kwa vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa.

Sheha huyo  amesema hatua mbalimbali ameweza kuzichukua katika kukabilia na  tatizo hilo la madawa lakini bado ipo haja kwa jeshi hilo la polisi kuongeza nguvu zaidi ili kuona vitendo hicho  vinaondoka katika shehia hiyo.

Hata hivyo amekiomba kitengo cha madawa ya kulevya Zanzibar  kutoa elimu kwa vijana juu ya athari za utumiaji wa  madawa hayo.

Amina Omar