Mahakama ya vileo Zanzibar yatoa tahadharia kwa wafanya biashara pombe

Mahakama ya Vileo Zanzibar imesema kutokana na kuwepo kwa baadhi ya malalamiko kwa wananchi juu ya baa zinazokiuka taratibu na sheria zilizowekwa  hivyo wameandaa operesheni maalumu  kwa  baa zote zinazouza  vileo.

Akizungumza na Zanzibar24  Katibu wa Mahakama hiyo Saleh Ali Abdalla amesema  katika operesheni hiyo itayofanywa hawatasita kuwachukulia hatua kali za kisheri  ikiwemo  kuwafungia biashara hizo wa  miliki wa baa ambao  hafuati kanuni na taratibu zilizowekwa.

Amesema Miongoni mwa  sababu za kufungiwa mtu biashara yake ya pombe ni kukosa sifa za usafi katika eneo lake la kuuzia biashara,kupiga mziki kwa sauti kubwa,baa kuwa karibu na nyumba za ibada,kutokuzingatia umri wa wateja wake baa hiyo hufungiwa ili kulinda usalama wa raia.

Aidha  Mahakama ya vileo Zanzibar  imewataka wananchi kuzidisha mashirikiano kwa watendaji wa mahakama hiyo wanapona kuna  ukiukwaji wa sheria kuwa wawazi kusema katika  sehemu husika ili hatua zichukuliwe.

Hata hivyo Katibu huyo  amewataka wafanyabiashara wa pombe  kuwacha tabia ya kupiga mziki kwa sauti kubwa na kuzingatia wakati wa kufunga na kufungua ili kuepusha malalamiko kwa wananchi ambapo pia amelitaka jeshi la polisi  kutosita kuwachukulia hatua wamiliki wa baa wanaokaidi.

Amesema Mahakama inamamlaka ya kuwapokonya Vibali wamiliki wa baa ambao hawafuati sheria zilizowekwa pamoja na kufunga biashara hiyo hivyo ili kuepusha hayo wafanyabiashara wafate  utaratibu kabla hawajaanza kuchukuliwa hatua za kisheria.

Amina Omar