Umwagaji wa taka katika mitaro ya maji machafu utaweza kuleta mafuriko Zanzibar

Wananchi  wanaoishi  karibu na mitaro ya kupitishia maji machafu wametakiwa  kuwacha tabia ya kumwaga taka katika kitaro hiyo kwani wanaweza kusababisha maji kutuwama na kupelekea maji hayo kuingia katika nyumba zao kusababisha mafuriko.

Akizungumza na Zanzibar24   Sheha wa Shehia ya Miembeni Haji Shomari Haji amesema  kitendo cha wananchi kumwaga taka katika mitaro kuna uwezekano mkubwa  wananchi wa shehia yake kuingiliwa na maji katika nyumba zao kutokana maji yale yanashindwa kupita na kwenda katika sehemu husika.

Amesema  kuwa pia mtarao huo huzidiwa pindi mvua zikiwa kubwa kutokana mtaro huo kuwa mdogo na kuwataka wananchi kuwa tabia za kumwaga taka katika mtaro huo ili kujiepusha na majanga yanayoweza kuepukika na badala yake wakatupe taka katika maeneo ya kumwagia taka.

Akizungumzia suala la utunzaji wa mazingira amesema wananchi wake wamekuwa na muamko mkubwa wa kutunza na kuhifadhi mazingira kutokana na elimu ya mara kwa mara wanayopewa juu ya ugonjwa wa kipindupindu.

Amina Omar