Ali Kiba Afunguka Sababu za Kuoa Mrembo wa Kenya Leo

Unafahamu sababu ya Alikiba kufunga ndoa siku ya leo? Basi unatakiwa kufahamu kuwa mtoto wa nyoka ni nyoka tu hawezi kuwa mjusi.

Sababu ya msanii huyo kufunga ndoa siku ya leo ni kutokana na kufuata nyayo za wazazi wake ambao walifunga ndoa siku kama ya leo miaka mingi iliyopita.

Hilo amelithibitisha Alikiba kupitia mtandao wake wa Instagram.

Kupitia mtandao huo Kiba ameandika, “Siku ya leo Ndio Siku Mama Yangu Na Baba Yangu walifunga Ndoa ALHAMDULILAH #KingKiba.”

Alikiba amefunga ndoa alfajiri ya leo (Alhamisi) ya April 19 huko mjini Mombasa nchini Kenya na mrembo Aminah Rikesh Ahmed. Hata hivyo sherehe nyingine kubwa ya ndoa hiyo inatarajiwa kufanyika siku chache zijazo jijini Dar es Salaam.

Mzazi mwenziwe na Ali Kiba afunguka ya moyoni

Tazamapicha harusi ya Ali Kiba: