Waandishi wa habari washauriwa kutumia mitandao ya kijamii

Waandishi wa habari wameshauriwa kutumia mitandao ya kijamii katika kuandika habari zao ili kuongeza nguvu za kupaza sauti za wananchi juu ya matatizo yanayowakabili  kwa lengo la kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa kutoka chama cha wanahabari wanawake Tanzania (Tamwa-Zanzibar) Asha Abdi Makame katika Mafunzo ya siku moja jinsi ya waandishi kuona umuhimu wa kutumia mitandao ya kijamii katika kuandika habari zao.

Alieleza kuwa wananchi wanamatatizo mengi yanayowakabili na endapo waandishi wa habari watatumia vyema mitandao  ya kijamii ikiwemo  twitter  facebook,whatssap   kwa kuunganyisha na vyombo vyao  vya   habari ikiwemo redio,tv na magazeti matatizo yaliomo katika jamii yanaweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka kwani kutakuwa na nguvu pamoja na kasi ya vyombo hivyo  kwa kutoa  msukumo kwa viongozi kuwajibika.

“Leo mtu wa chini hajui anahaki gani katika serikali  za mitaa lakini  mkitumia mitandao ya kijamii na mkawafahamisha juu ya hilo basi wataelewa na kudai haki zao”  alieleza Asha.

Alieleza kuwa ili dhana  ya uwajibikaji iweze kufikiwa na kuleta tija  katika jamii ni vyemaa wananchi kushirikishwa shughuli mbali mbali ziwe za jamii na katika ngazi maamuzi.

“Unapowasemea wanyonge  mtakuwa  mmetimiza ile dhana ya tasnia  yenu ya kuwasemea wasiokuwa na sauti” alieleza Asha.

Akifunga Mafunzo hayo Naibu Mkurugenzi wa habari  Maelezo Juma Muhamed Salum ameitaka Jumuiya  ya waandishi wa habari za maendeleo Zanzibar  wahamaza kuwapatia mafunzo Viongozi wa Serikali na wajumbe wa baraza la wakilishi juu ya umuhimu wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutangaza kazi zao.

“Ni  vyema Wahamaza baada ya kuwapatia mafunzo haya waandishi , mjipange kuwapatia mafunzo Viongozi wetu kwani jamii wanahitaji kujuaa nini wanafanya” alieleza Naibu huyo.

Alisema kuwa Mitandao ya kijamii mbali na kurahisisha habari kufika kwa urahisi na haraka lakini wako baadhi  wengine hutumia mitandao kinyume na malengo yake ambapo hupelekea uvunjifu  wa amani.

Mapema katibu mkuu wa Jumuiya ya waandishi wa Habari za maendeleo Zanzibar (Wahamaza) Salma Said aliwaambia waandishi wa habari muda  umefika kuunganisha taarifa zao kwenye mitandao ya kijamii ili kuwa na wasomaji  wengi zaidi.

Mafunzo hayo yamendaliwa na Jumuiya ya waandishi wa habari za Manendeleo Zanzibar (Wahamaza) ambayo ni mshiriki mmojawapo wa watekelezaji wa mradi wa kuinua uwajibikaji katika mpango wa ugatuaji wa madaraka Zanzibar. Washiriki wengine katika mradi huo unaofadhiliwa na ZANSAZP, ni Tamwa na Jumuia ya Kuhifadhi maliasili za asili Pemba {NGERANECO}.

Amina Omar