Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imeweka rekodi nyingine baada ya leo kupokea meli kubwa zaidi

Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imeweka rekodi nyingine baada ya leo kupokea meli kubwa zaidi ya Northern Power yenye urefu wa mita 265 ambayo imetia nanga Bandari ya Dar es Salaam  kwa ajili ya kupakuwa mizigo.

Hatua hiyo ni muendelezo wa kuongeza ufanisi wa bandari hiyo katika kutoa huduma na kupunguza ushindani unaoupata kutoka katika bandari za jirani za Durban na Mombasa.

Kwa siku za hivi karibuni serikali imekuwa ikifanya jitihada za makusudi kupanua Bandari ya Dar es Salaam lakini pia kuongeza kina cha maji ili iweze kuhudumia meli nyingi na kubwa zaidi. Hatua hiyo itawezesha wateja wengi wa Tanzania na nje ya nchi kutumia bandari hiyo kupitisha mizigo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), meli hiyo ina uwezo wa kubeba makontena ya mizigo zaidi ya 5,000 kwa wakati mmoja.

Akizungumza Bandarini DSM Mkurugenzi wa shughuli za Meli, Yusuph Mwingamnoamesema “Wasafrishaji wa meli wanapenda kutumia meli kubwa kuepuka gharama, nikiwa na maana kwamba Mombasa na Durban wao bandari zao ni kubwa wanaingiza meli kubwa kuliko zinanzoingia DSM, maanake ni kwamba wafanyabiashara wengi watakuwa wanachukua mizigo nje wanapeleka kwao, halafu sisi tuchukue kwao kwa vimeli vidogo na vimeli vidogo vinalipa kidogo”

Hapa chini ni picha za meli hiyo;