Sita usiyoyajua kuhusu Chumvi

Sote tunajua kuwa ulaji wa chumvi kwa wingi ni hatari kwa afya zetu, ingawa wengi wetu bado ni watumiaji wakubwa wa chumvi, lakini je wajua kuwa huwezi kuishi bila chumvi?

1.Tunakuletea orodha ya mambo sita usiyoyajua kuhusu chumvi:Neno ‘Salary‘ ambalo kwa kiswahili ni mshahara linatokana na neno Salt (Chumvi).  Katika enzi za kale, chumvi ilikua ni kitu cha thamani kubwa kiasi kwamba malipo ya kila mwezi ya mshahara yalihusishwa na mahitaji ya kununua chumvi. Neno mshahara limetokana na neno la kilatini ‘Salarium’, lililokuwa na maana yaana malipo kwa askari wa ili waweze kujinunulia chumvi.

2. Chumvi ambayo humwagwa barabarani ni nyingi zaidi kuliko inayotumika kwenye chakula. Nchini Marekani ni asilimia 6 tu ya chumvi inayozalishwa hutumika kwenye chakula na asilimia 15 humwagwa barabarani kipindi cha baridi ili kuondosha mabarafu.

3. Inaaminika kwamba ukimwaga chumvi unajilietea mkosi. Imani hii ilitokana na mchoro ulioitwa ‘The Last Supper’ uliochorwa na Leonardo da Vinci, katika mchoro huo unamuonesha Judas Iscariot (aliyemsaliti Yesu ambaye badae alijinyonga) akipiga bakuli la chumvi.

4. Chumvi inaweza kuua: Kama utakula gram ya chumvi kwa kila kilo ya mwili wako, mathalan kama una kilo 50 na ukala gram 50, basi unaweza kupoteza maisha. Hapo kale katika nchi ya China, kula kiasi kinachokadiriwa kwa ni nusu kilo ya chumvi ndio ilikua njia inayopendelewa ya kujiua kwa watu wenye heshima zao. Chumvi ilikua ni ghali sana wakati huo, hivyo ni vigogog tu ndio waliweza kununua chumvi ya kutosha kuweza kujiua.

5. Chumvi ya bahari yenye kiwango ni lazima iwe na unyevunyevu tofauti na chumvi za viwandani ambazo tayari zimeondolewa madini mengi. Chumvi nzuri ya bahari ina madini mengi yanayohitajika katika mwili wa binadamu.

6. Kuna Hotel nchini Bolivia imejengwa kwa kutumia chumvi. Palacio de Sal resort imejengwa yote kwa matofali ya chumvi. Hawakuishia kwenye matofali viti, meza, vitanda na hata bwawa la kuogelea, vyote hivyo vimetengezwa kwa chumvi.