Alichosema Haji Manara kuhusu kuondoka Simba

 

Kufuatia ujumbe tata aliopost Msemaji wa Timu ya Simba Haji Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram hapo jana usiku ambao umezua mjadala miongoni mwa watu, mapema leo  May 2, 2018 Haji Manara, amewatoa hofu mashabiki wa Simba kwa kuweka wazi kuwa hana mpango wa kuondoka katika timu hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram, Manara amesema kuwa “Siondoki Simba na naomba muelewe hvyo..ninafanya kazi sehemu sahihi na wakati sahihi….rafiki zangu na washabiki wa klabu muelewe hvyo..walichokitangaza ni uzushi…nawezaje kuwaacha simba kipindi hiki muhimu”?

hapo jana Manara alipost ujumbe uliokuwa na utata na kupelekea baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kwamba huenda kuna kutofautiana kati ya Manara  na uongozi wa juu wa Simba huku baadhi ya watu walianza kujiuliza maswali kadha wa kadha na wengine kuhisi kwamba Manara ana mpango wa kuiacha timu yake ya Simba.

Jana Manara aliandika “Nia yangu ni njema sana lakini na mimi nina nyongo sihitaji heshima ila walau nipewe utu ninaostahili nimefanya kwa kadiri nilivyojaaliwa a Mungu ila lazima tusonge mbele kwa maslahi mapana ya klabu.” Ujumbe ambao ulizua maswali miongoni mwa watu.