Hizi hapa Bei mpya za Mafuta Zanzibar

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma, Nishati na Maji Zanzibar ZURA  imetoa taarifa juu ya bei za mafuta zitakazoanza kutumika rasmi kuanzia leo Jumanne ya tarehe 8-5-2018. Bei hizo ni kama ifuatavyo:

Bei ya reja reja ya Mafuta ya petrol itakua ni shilingi 2,255 kwa lita badala ya shilingi 2,344 ya hapo awali

Bei ya reja reja ya Mafuta ya Dizeli itakua ni shilingi 2,250 kwa lita badala ya shilingi 2,314 ya hapo awali

Bei ya reja reja ya Mafuta ya Taa itakua ni ile ile ya shilingi 1,740 kwa lita

Bei ya reja reja ya Mafuta ya Banka itakua ni shilingi 2,078 kwa lita badala ya shilingi 2,156 ya hapo awali

Bei ya reja reja ya mafuta ya Ndege itakua ni 1,810.21 kwa lita badala ya shilingi 1812.63 ya hapo awali