Maalim Seif ameitaka SMZ kupunguza kodi kwa wafanyabiashara

Katibu Mkuu wa Chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamada amewataka wafanyabiashara wa vyakula, nguo na vifaa vinavyotumika kwa matumizi mbalimbali kuacha tabia ya kupandisha bei ya bidhaa hizo katika mwezi mtukufu wa ramadhani.

Akizungumza na Waandishi wa habari amesema mbali na wafanyabiashara kuwataka kushusha bei za bidhaa zao lakini pia ameiomba serikali  nayo kushusha kodi kwa wafanyabiashara hao ili kuweza kuuza bidhaa zao kwa unafuu katika kipindi hichi.

Hata hivyo Maalimu Seif amewataka wananchi  kuukaribisha mwezi wa ramadhani kwa kufanya mambo ya kheri nakuacha kufanya matendo yatakayo mkera Allah (s.w)

Amesema wapo baadhi ya wananchi  hufanya kwa makusudi matendo yanayomchukiza Mungu hivyo amewataka wananchi hao kuwacha na endapo watakaidi kwa kufanya matendo maovu hadharani basi vyombo husika viwachukulie hatua za kisheria.

Amina Omar.