Nafasi 12 za kazi katika Idara ya Serikali Mtandao Zanzibar

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Idara ya Serikakali Mtandao kama ifuatavyo:-

1.BUSINESS ANALYST DARAJA LA II – Nafasi tatu (3) Unguja.

Sifa za Muombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Computer Science, Information Systems au Information Technology kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2.SYSTEM DEVELOPER/PROGRAMMER DARAJA LA II Nafasi tatu(3) Unguja.

Sifa za Muombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Computer Science, Information Systems au Information Technology kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3.ICT SECURIRY/ AUDITOR DARAJA LA II – Nafasi moja (1) Unguja.

Sifa za Muombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza katika fani ya Computer Science au Information Security kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4.IT PROJECT OFFICER DARAJA LA II – Nafasi moja (1) Unguja.

Sifa za Muombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza katika fani ya Computer Science kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza katika fani IT Project Management Methology kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5.DATA BASE ADMINISTRATER DARAJA LA II – Nafasi moja (1) Unguja.

Sifa za Muombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya shahada ya kwanza katika fani ya Computer Science au Information Technology kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6.LEGAL OFFICER DARAJA LA II – Nafasi moja (1) Unguja.

Sifa za Muombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza fani ya Cyber Law kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

7.ICT OFFICER DARAJA LA II – Nafasi mbili (2) Pemba.

Sifa za Muombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza fani ya Computer Science, Information Technology kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 – ZANZIBAR.

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 18 Mei, 2018 wakati wa saa za kazi.