DC Rajab Ali atoa onyo kwa watenda maovu mwezi wa ramadhani

Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja Rajab Ali Rajab amesema hato mvumilia mwananchi yeyote atakaye kwenda kinyume na kufanya matendo yanayomchukiza mwenyezi mungu  katika Mwezi mtukufu wa ramadhani.

Akizungumza na Zanzibar24  amesema  anatambua kuwa wilaya yake imezungukwa na ukanda wa pwani na baadhi ya watu huutumia kwa kufanya matendo yao maovu hivyo amejipanga kikamilifu kuwachukulia hatua watu watakaobainika kufanya maovu katika mwezi huu mtukufu.

Amina Omar