Hili hapa jina jipya la Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani

Kwa mujibu wa Kifungu Namba 4(1) cha Sheria ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa Namba 10 ya mwaka 2002, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein ametangaza Kuwa Ukumbi Uliokuwa Baraza la Wawakilishi la Zamani (Kikwajuni) Umepewa Heshima ya Kuitwa Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil.

Lengo Kuu la Ukumbi Huo Kupewa Jina Hilo ni Kwa Madhumuni ya Kumuenzi Marehemu Sheikh Idrissa Abdul Wakil aliyekuwa Rais wa Zanzibar wa Awamu ya Nne na Spika wa Mwanzo wa Baraza la Wawakilishi.

Kadhalika, kwa Mujibu wa Kifungu Namba 4(2) cha Sheria ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa Namba 10 ya mwaka 2002, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Ameruhusu Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Kuitwa Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein.

Lengo Kuu la Kuupa Ukumbi Huo Jina la Dkt. Ali Mohamed Shein ni Kumuenzi na Kutambua Mchango wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Katika Kukuza Elimu.

Majina Hayo Yataanza Kutumika Rasmi Kuanzia Tarehe 11 Mei, 2018.