Mtoto wa miaka 8 akutwa kichakani akiwa amefariki Unguja 

Mtoto Elizabeti Ndaula mwenye umri wa miaka 8 amekutwa ameshafariki katika kichaka Mtaa wa Bambi Mkoa wa Kusini Unguja.

Sheha wa Shehia ya Bambi Amour Pandu Mkombe amesema kuwa marehemu huyo baada ya kifo chake alikua akirudi skuli pamoja na wenziwe ndipo ambapo walipopoteana kwa mazingira ya kutatanisha pamoja na kutafutwa huku wakitoa taarifa kwenye vituo vya Polisi mbalimbali na kuonekana kwa siku ya pili kichakani akiwa ameshafariki.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna msaidizi wa Polisi Makarani Khamis Ahmed amesema kuwa kutokana na taarifa walizozipata kutokana na kifo cha mtoto huyo imewahamasisha kufungua jalada la uchunguzi ili kubaini kifo hicho kimesababishwa na kitu gani.