Mwakilishi wa Magomeni alia na vijana wa jimbo lake

Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi amesikitishwa na muamko mdogo wa  vijana katika jimbo lake kushindwa kuitumia fursa ya kielimu  katika kujiendeleza katika fani mbalimbali  badala yake hukaa mitaani na  kusikitika  kuwa hawana ajira.

Akizungumza na Zanzibar24 amesema  miongoni mwa mikakati yake katika jimbo lake ni kuwaendeleza vijana mia 100 kielimu  kwa  fani za ujasiriamali, hotelia, Vikundi vya saccos  lakini  vijana  wamekuwa na muitikie mdogo kujitokeza kuitikia   fursa hizo na  hadi sasa ni vijana 35 tu  ndio waliojitokeza.

Amina Omar