Raia wa Malawi akutwa na dawa za kulevya Uwanja wa Ndege wa  kimataifa Zanzibar

Mkuu wa kitengo cha Uwanja wa ndege Mrakibu wa Polisi Omar Khamis amemtaja mtuhumiwa huyo kwajina la Ester Kizungu mwenye umri wa miaka 31 ambae ni Raia wa Malawi.

“Amekamatwa akiwa anataka kusafiri kuelekea India, aliingia Tanzania kutokea Malawi tarehe 6 mwezi wa 5 ambapo tarehe 13 akaingia Zanzibar kutokea Dar ess salaam ndipo alipowasili moja kwa moja uwanja wa ndege majira ya saa 6 mchana hapo ndipo alipokamatwa akiwa na unga wa madawa ya kulevya katika mifuko miwaili tofauti iliyokuwa na inauzito unaokadiriwa kuwa na kilo 3.5”Amesema Mrakibu huyo.

Omar ametoa wito kwa jamii kuwa vita vya madawa ya kulevya ni vita vya wote kwahiyo wananchi kwa ujumla wanapaswa kushirikiana na kwa kutoa taarika ndani ya vyombo husika ambapo wanapobaini tatizo kama hilo.