SMZ yazungumzia uwepo wa ugonjwa wa Chikungunya

Wizara ya afya imewatoa hofu wananchi wa Zanzibar juu ya ugonjwa wa Chikungunya kwamba  wauchukulie wa kawaida kama magonjwa mengine kwani sio hatarishi  na endapo  watadumisha usafi katika  maeneo yao wataweza kuepukana ugonjwa huo.

Akizungumza na Zanzibar24 Naibu Waziri wa Wizara hiyo Harusi Said Suleiman amesema serikali chini ya wizara ya afya inaufahamu ugonjwa  wa chikungunya  ambao unasababishwa  na mbu na hakuna athari kubwa zilizotokea  juu ya ugonjwa huo na wapo baadhi ya wananchi wameupata ugonjwa huo na matibabu yake yanapatikana katika vituo vya afya pamoja na hospital kuu ya Mnazimmoja.

Hata hivyo Naibu Harusi ametoa wito kwa hospitali binafsi kuwahudumia  wagonjwa  kama zilivyosheria  za serikali  na kuwacha tabia za kuwapa hofu wananchi juu ya ugonjwa huo.

Amina Omar