Video: Vita ya Kamanda Nassir kwa wanaume wenye kujikohoza wanapokatizwa na wanawake yazua neno Baraza la wawakilishi

Kauli ya kamanda wa Polisi mkoa wa mjini magharib Unguja Hassan Nassir ali, aliyetangaza vita na wanaume wenye tabia za kujikohoza wanapokatizwa na wanawake wenye maumbile makubwa, imemuibua mwakilishi wa jimbo la Chaani Mhe. Nadir ABdul latif (CCM).

Kamanda Nassir alitoa kauli hiyo Jumatatu May 14, 2018, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Madema na kusema atawachukulia hatua wanaume wenye tabia za kujikohoza wanapokatizwa na wanawake wenye maumbile makubwa kwa kusema kitendo wanachokifanya ni ‘Shambulio la aibu’

Vita ya Kamanda Nassir na wanaume wenye kujikohoza wakikatizwa na wanawake yamuibua Mwakilishi Nadir ABdul latif.

 

Video: Kauli ya kamanda Nassir kwa wanaume wenye kujikohoza wanapokatizwa na wanawake wenye maumbile makubwa.