Wizara ya Afya yaweka huduma ya usafishaji damu

Wizara ya Afya Zanzibar imesema inaweka huduma ya Usafishaji wa damu (dielysis) katika Hospitali za Mkoa ili kuwawezesha wagonjwa wa figo kunufaika na huduma hiyo katika hospitali zilizo karibu na Makazi yao.

Akijibu swali katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogio ya mji wa Zanzibar Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Harusi Saidi Suleiman amesema serikali inatambua usumbufu wanaopata wagonjwa wakati wa kutafuta huduma hiyo kwa masafa marefu.

Amesema pia wagonjwa wanatumia gharama kubwa kufuata huduma hiyo katika hospitali Binafsi na kulazimika kulipa shilingi 250,000 jambo ambalo linawakosesha fursa ya matibabu kwa wakati hususan kwa wanachi wenye kipato cha chini.

Amesema katika kukabiliana na tatizo hilo tayari Wizara ya afya inaendelea na jitihada za kununua vifaa na kuengeza wataalamu watakaotoa huduma ya Dielysis kwa wagonjwa wa figo kuwawezesha wagonjwa kupata matibabu kwa gharama nafuu.

Na;Fat-hiya Shehe Zanzibar24.