Mtoto afariki baada ya nyumba yao kujaa maji Unguja

Mtoto mmoja afariki baada kutumbukia ndani ya maji kufuatia nyumba yao kujaa maji na kufurika.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 8 za usiku huku mvua ikiemdelea kunyesha huko Mtoni Kidatu Wilaya ya Magharib A Unguja.

Baadhi ya Mashuhuda walioshuhudia tukia hilo wamesema kuwa maji yalikuwa yanaingia ndani kwa kasi na kujaa ambapo milango ilikua haifunguki wakati walipokua wakijihami kukaa juu ya dari mtoto huyo alimponyoka kwa yule ambae aliemshika na hatimae kuzidiwa na maji.

“Yule mtoto mdogo alikuwa amepewa mwenziwe amkamate lakini kwa bahati mbaya akamuanguka na maji yalikua ni mengi”Amesema mmoja kati ya shuhuda hao.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Sheha wa Shehia ya Mtoni Kidatu Muki Makame Ussi amesema walifanya juhudi ya kumtafuta mtoto huyo hatimae walipomuona tayari walimkuta ameshafariki.

Kwaupande wake Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Saidi Juma Ahmada amewapa pole wazazi wa mtoto huyo kuwa wawe na moyo wa subra kwani msiba huo ni msiba wa wote.