Ramadhani yaleta sura mpya ya bei za bidhaa sokoni Mwanakwerekwe

Leo may 17, 2018 sawa na mwezi mosi ramadhani, Waumini wa dini ya kiislamu kote duniani waungana kutimiza nguzo ya 4 ya kiislamu inayowalazimu kujizuia kula, kunywa na mambo yote maovu kwa muda maalum.

Ni kawaida ya watu unapofika muda wa kufutari huandaa vyakula vingi vya aina mbalimbali kwaajili ya familia zao.

kwa kuliona hilo Zanzibar24 imetembelea soko kuu la Mwanakwerekwe Zanzibar kuangalia bei ya baadhi ya bidhaa maarufu zinazopendwa ndani ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ambapo:

  • Nazi Tsh. 1,000=/ hadi Tsh. 1,300=/
  • Majimbi, Muhogo, Viazi vitamu vinauzwa Tsh.2,000=/ hadi 5,000=/ kwa fungu.
  • Viazi vikuu fungu Tsh. 5,000=/
  • Ndizi mbivu chana Tsh. 4,500=/ dole Tsh. 1,000 hadi Tsh. 2,000=/
  • Viazi Mbatata kilo Tsh. 1,000=/
  • Boga Tsh. 3,000=/
  • Njugu mawe kilo Tsh. 3,000=/ na
  • Tambi kilo Tsh. 2,400=/

Zanzibar24 inawatakia kheri ya mfungo wa ramadhani waislamu wote duniani.