Baraza la wawakilishi Zanzibar lapitisha Bajeti ya mwaka 2018/2019

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamepitisha Bajeti ya Wizara ya katiba, Sheria ,utumishi wa Umma na Utawala bora ya mwaka 2018/19 na kuitaka serikali kuharakisha utatuzi wa kesi.

Akizungumza katika Ukumbi wa baraza la wawakilishi Mwanasheria mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Saidi Hassan Saidi amesema watahakikisha wananchi na Watendaji wa Serikali wanafuata sheria ya Nchi ili kuweka haki sawa.

Amesema ni kweli kuna mamalalmiko makubwa kwa baadhi wananchi kukosa haki zao hasa katika kesi za Udhalilishaji hivyo wataendelea kufanya kazi kwa sheria ili kuwawezesha wananchi kutatuliwa kesi zao kwa muda mfupi.

 Waziri katiba, Sheria ,utumishi wa Umma na Utawala bora Haroun Ali Suleiman amesema Ofisi yake itaendelea kusimamia majukumu walinayo katika kufikisha huduma bora kwa wananchi ili kuimarisha maendeleo Nchini.

Amesema serikali inatambua baadhi ya matatizo yanayowakabili wananchi hivyo yataendelea kupatiwa ufumbuzi ili kutekeza utawala bora kwa kuzingatia Sheria.

Akizungumzia suala la kuzuia Rushwa Waziri Haroun  amesema kupitia Mamlaka ya kuzuia rusha na uhujumu Uchumi itaendelea kuwachukulia hatua za kisheria mwananchi yoyote atakae husika na kitendo cha rushwa bila kujali Cheo wala nafasi alinayo katika jamii.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamepitisha Shillingi 27,587,100,000.00 kwa wizara hiyo fedha ambazo zitatumika katika utekelezaji wa majukumu ya wizara hiyo.