Faiza Ally afunguka tuhuma za kuchepuka na mume wa mtu

Msanii wa Filamu Bongo, Faiza Ally amefunguka sababu ya kutomuweka hadharani mzazi mwenzie wa sasa.

Muigizaji huyo amesema analazimika kutomuonyesha kwa sababu hawana malengo yoyote ila si kwamba ni mume wa mtu.

“Sipendi kumuonyesha sio sababu ni mume wa mtu, ni sababu hatuna malengo, hatutegemei kuoana wala kuishi pamoja kwa hiyo i take my time, when time come kuonyesha kwenye media nitafanya hivyo,” Faiza ameiambia Bongo5.

Ameongeza kuwa aliamua kuzaa mtoto wa pili kwa sababu umri unaenda na malengo yake yalikuwa akifikisha miaka 35 tayari awe na watoto na hao alionao wanamtosha.

Faiza ni mama wa watoto wawili, Sasha na Li Junior.