Hiki ndio kikosi cha Ufaransa kitakacho cheza Kombe la Dunia

Kocha Didier Deschamps wa timu ya taifa ya Ufaransa ametangaza kikosi cha wachezaji wake 23 ambao wataenda kucheza michuano ya kombe la dunia itakayofanyika Urusi mwezi Juni mwaka huu.

Deschamps amewashangaza mashabiki wa soka duniani kwa kuwaacha baadhi ya wachezaji ambao wamezoeleka kwenye kikosi hiko akiwemo Alexandre Lacazette (Arsenal),Kingsley Coman (Bayern Munich), Dimitri Payet (Olympique de Marseille), Anthony Martial (Manchester United) na Karim Benzema (Real Madrid).

Akitangaza majina hayo kupitia kituo cha runinga cha French TV Alhamisi hii usiku, kocha huyo ametaja miongoni mwa majina ya wachezaji aliowateua ni Hugo Lloris, Alphonse Areola, Mandanda, Umtiti, Mendy, Varane, Hernandez, Kimpembe, Rami, Sidibe na Pavard.

Wengine ni N’Golo Kante, Paul Pogba, N’zonzi, Tolisso, Matuidi, Kylian Mbappe, Ousmane Dembele, Giroud, Nabil Fekir, Thomas Lemar, Antoine Griezmann na Florian Thauvin.