Serikali yaa hidi kumaliza migogoro ya ardhi zanzibar

Wiraza ya Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati kwa kushirikiana  na Serikali imesema itahakikisha inaitafutiwa ufumbuzi migogoro ya ardhi kwa kufuata sheri zilizopo ili kila mtu aweze  kupata haki yake  ya msingi.

Akizungumza na Zanzibar24  Naibu Waziri wa Wizara hiyo  Juma Makungu amesema serikali inatambua kuwa Zanzibar katika wilaya mbalimbali migogoro bado ipo na isipodhibitiwa kwa mujibu wa sheria  itaweza kupelekea vurugu kwa wananchi,wawekezaji na serikali.

Aidha makungu amewataka wananchi kufuata sheria katika kutatua migogoro yao pamoja na kuitumia kamisheni ya ardhi ili kuweza kusaidia juu ya mgogoro.

Amina Omar