TRA  yaahidi kutoa elimu kwa wananchi  na wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kulipa kodi

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imesema itaendelea kutoa elimu kwa wananchi  hususani kwa wafanyabiashara juu ya kulipa umuhimu suala la kulipa kodi kwa wakati kwani fedha hizo hutumika katika kuharakisha maendeleo ya nchi.

Akizungumza na Zanzibar24  Afisa Elimu na huduma kwa mlipa kodi Abdalla Seif amesema licha ya kutolewa elimu kwa wafanyabiashara katika kulipa kodi lakini wapo baadhi ya wafanyabishara hawatoi risiti wanapoudha bidhaa zao kwa mteja jambo ambalo nikosa kisheria.

Hata hivyo amesemaTRA itamchukulia hatua za kisheria  mfanyabiashara yoyote atakaegundulika kuwa halipi  kodi kwani kufanya hivyo ni kuikosesha serikali mapato yake.

Amina Omar