Dulla Makabila afunguka kwa mara ya kwanza kujibu tuhuma za kubaka Mwanafunzi

Msanii maarufu wa singeli Dulla Makabila amekanusha tuhuma zinazomkabili za kubaka Mwanafunzi kwa kusema kuwa hajabaka na hana kesi Polisi kama ambavyo tetesi zinasema.

Msanii huyo amesema kuwa amekuwa akipokea simu nyingi pamoja na familia yake kwa tuhuma ambazo amedai sio kweli na zinapelekea migogoro na mkewe.

“Mambo ya kuzushiwa ni mengi sana hali inayopelekea muda mwingine ugomvi na mke wangu, nimepokea simu nyingi sana kuhusu hilo tukio la kuhusishwa kwenye tuhuma za kubaka lakini mimi nilikuwa mikoani kwenye kazi zangu taarifa hazina ukweli wowote” amesema Makabila kupitia eNewz ya EATV.

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi zilizosambaa kupitia mitandao ya kijamii kuwa msanii huyo amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kubaka mwanafunzi.