Harmonize kukutana na Ex-Girlfriend wake siku ya Eid Pili

Msanii wa muziki kutoka WCB, Harmonize leo ametambulisha Usiku wa Kusi utakaofanyika siku ya Idd Pili katika Ukumbi wa Dar Live ambapo atakutana na ex-girlfriend wake Jackline Wolper .

Akizungumza na waandishi wa habari leo June 05, 2018 Dar es Salaam, Harmonize amesema kuwa amemchangua Wolper kufanya hivyo ni kutokana anaweza hilo na kuonesha hakuna tofauti kati yao.

“Wolper ana uwezo wa ku-host show, kwa sababu ameshazoea sana mambo haya, pengine kwenye movie wako location, halafu pili kitu kingine Wolper ana fan base kubwa naamini ataweza kuisimamia show vizuri,” amesema.

“Lengo ni kuwaonesha watu kuwa hatuna tatizo mimi na yeye na tunashirikiana katika kazi, hii yote tunaepusha kuwagawa mashabiki, yeye ana mashabiki zake na mimi nina wangu,” amesisitiza.

Utakumbuka Harmonize na Wolper walikuwa katika bifu zito kitu kilichopelekea kutupiana maneno katika mitandao na kwenda mbali zaidi hadi kumuhusisha mpenzi wa sasa wa Harmonize, Sarah.