Orodha ya vyakula 10 vyenye kuongeza nguvu na kuimarisha kinga ya mwili

Hivi ni vyakula vinavyoweza kukusaidia kuongeza kinga ya Mwili wako.

1.Yogurt ( Maziwa mtindi )

Maziwa Mtindi

Hutengenezwa kwa kutumia maziwa ya ng’ombe na kimea, hupatikana kwa ladha mbalimbali kulingana na matakwa yako, yogati pengine ndio chakula kinachoongoza kwa kuogeza Kinga ya mwili wako na husaidia kuukinga mwili wako na magonjwa kama UTI, Fangasi na mengineo .

2. Matunda

Aina mbalimbali za Matunda

Yanapatikana sehemu yoyote duniani kwa bei unazozimudu, katika mlo wako wowote jitahidi usiache kujumuisha angalau tunda la aina moja. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, asiyekula matunda anahatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa zaidi ya mlaji wa matunda.

3. Vitunguu saumu

Vitunguu saumu

Hupatikana Kila soko Tanzania! Japokuwa vitunguu saumu vimekuwa vikitumika sana kwa ajili ya matibabu ya magonjwa mbalimbali toka enzi za mababu, wataalamu wameshauri pia vitunguu hivi ni chanzo muhimu kwa kinga ya binadamu. Vitumie kwa kutafuna (kama unaweza) au weka kwenye chakula!

4. Uyoga

Uyoga

Usishangae! Ndio.. hiki ni moja ya vyakula muhimu zaidi kuimarisha afya yako kwani huchangia kiasi kikubwa kuimarisha seli nyeupe za damu zinazofanya kazi ya kupambana na magonjwa mbalimbali!

5. Supu ya kuku

Supu ya Kuku

Wengi watahisi ni gharama lakini si kubwa kuzidi gharama ya kumuona daktari! Unywaji wa supu ya kuku ya moto  husaidia kuzuia kupungua kwa seli nyeupe za damu vilevile hupunguza uwezekano wa kupata matatizo yanayohusiana na mapafu na mfumo wa hewa kiujumla!

6. Viazi vitamu

Viazi Vitamu

Unaweza kuhisi ngozi sio sehemu ya muhimu katika kinga ya binadamu lakini ukweli ni kwamba  ngozi ni sehemu ya muhimu sana kwa mwili wa binadamu. Kwa kinga kamili ya mwili wa binadamu tunahitaji Vitamin A ambayo hupatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu.

7. Karoti

Karoti

Karoti zina ziada kubwa ya vitamin pengine kuliko tunda lolote lile hivyo jitahidi kujumuisha karoti kama kiungo kwenye chakula au unaweza kuitafuna ikiwa mbichi!

8. Samaki

Samaki

Husaidia seli nyeupe kuzalisha ctokins zinatohusika kuzuia baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na virusi hasa yale yanayohusiana na mfumo wa hewa nk.

9. Matikiti

Matikiti

Wengi Hudharau lakini tunda hili ni muhimu sana katika afya ya kila siku ya binadamu kwani husaidia kuongeza kiasi cha maji mwilin, madini chuma na kuimarisha seli nyeupe za damu

10. Maji

Maji

Kama kuna Kitu cha kwanza kwa uhai wa binadamu basi ni maji. Bila kunya maji ya kutosha bado utakuwa katika hatari ya kupata magonjwa mbalimbali. Angalau lita moja na nusu kwa siku ni muhimu kwa afya yako!