Mara paap, Wolper huyu hapa Show ya Harmonize ‘Kusi Night’

Baada ya msanii wa muziki, Harmonize kutangaza show yake ya ‘Kusi Night’ itakayofanyika Dar Live siku ya Eid Pili June 17, 2018 ambapo alisema kuwa ni Wolper atakuwa host wa show hiyo.

Muda mfupi baada ya Harmonize  kutoa kauli hiyo. Wolper kupitia ukurasawake wa instagram alijibu ambapo aliandika “NAOMBENI MTAMBUE KUWA SIPO TANZANIA NA SITOKUWEPO KWENYE SHOW YOYOTE” aliandika wolper.

Harmonize kukutana na Ex-Girlfriend wake siku ya Eid Pili

TANGAZO!! TANGAZO!!TANGAZO!!!..
NAOMBENI MTAMBUE KUWA SIPO TANZANIA NA SITOKUWEPO KWENYE SHOW YOYOTE.. IWE YA MBAGALA IWE YA POSTA MIMI KAMA WOLPER SIHUSIKII,
YOTE MNAYOYASIKIA WANAYASEMA NI YA UONGO WANATAKA KUWATAPELI
SITAKI MTU ATUMIE JINA LANGU KUVUTA WATU.
EPUKA MATAPELI
ASANTENI SANA…. #EPUKAMATAPELISUGU
#ACHENIKUTUMIAJINALANGUKUVUTAWATU
#SIPOTANZANIANASIRUDIMPAKAJULY🙏.NAWAPENDA SANA MASHABIKI ZANGU WOTE.

 

Alicho andika wema kupitia instagram yake