Mchezaji wa zamani Zanzibar Heroes, ataka viongozi wenye utaalamu wa soka ZFA

Chama cha mpira miguu Zanzibar kimetakiwa kuwa na utamaduni wa kuwatafuta watu wenye utaalamu wa soka ili kukuendesha chama hicho.

Akizungumza na Zanzibar24 Mchezaji wa Zamani wa Zanzibar Heros na timu ya Taifa ya Tanzania Abdalla Maulid amesema hayo baada ya kuona chama hicho kuyumba kwa muda mrefu na viongozi kubaki madarakani.

Aidha Abdalla Maulidi ameelezea udhaifu wa mpira wa Zanzibar kwa leo ni kukosa viongozi wa mpira kwenye ngazi ya vilabu kwa kutokuwa na elimu ya uongozi katika michezo.

Ameendelea kufafanua kwa kipindi kirefu tangu mwaka 2004 vilabu vya Zanzibar vimekuwa vikishindwa kuendelea kwenye Mashindano ya kimataifa yanayo andaliwa na CAF kwa kutoka raundi ya mwanzo ni kutokana na vilabu hivyo kutokuwa tayari kimashindano.

“Naliomba Baraza la Michezo Zanzibar chini ya mwenyekiti Rashid Gulam waandae kongamano la kitaifa kujadili mpira wa Zanzibar kwa ngazi ya vilabu umeshuka sana, Rashid Gulam yeye anajua mpira kacheza timu zote za Taifa namuomba sana” alisisitiza Abdalla Maulid.

Kwa upande mwengine Abdalla Maulidi amefunguka na kusema wachezaji wa zamani walitoa mchango wa soka la Zanzibar wametengwa kwa muda mrefu na chama cha mpira wa miguu Zanzibar kwani wao ndio wadau wa soka la Zanzibar.

“Wanahitaji msaada ZFA mwaka 1978 klabu ya KMKM imefika hatua ya nane bora  fainali ya kombe la shirikisho , Malindi wamefika hatua ya nusu fainali mwaka 1990 na Miembeni wamefika mzunguko wa pili miaka hiyo siyo leo tena” alifahamisha Abdalla Maulid.

 Abdalla Maulid mchezaji wa zamani wa klabu ya miemben na kmkm pia aliwahi kuchezea timu ya Taifa ya Zanzibar Hereos na na ile ya Taifa Stars amewataka ZFA kukaa pamoja na wachezaji wa zamani ili kujenga mpira wa Zanzibar .