Direct Aid wafanikisha mradi wa maji Mjini Magharibi

Mkuu wa mkoa wa mjini ndugu Ayubu Muhammed Mahmoud amelishukuru Shirika la Direct Aid kwa kutoa huduma za maji salama kwa mkoa wake wa mjini .

Hayo aliyesema wakati wa ufunguzi wa  mradi wa visima vya maji uliofanyika eneo la mwanakwerekwe ,wilaya ya mjini Magharibi  ndugu Ayubu amewataka skuli zinazofaidika na mradi huo mkubwa wa maji kuutunza ili kudumu .

Aidha amewashukuru shirika la Direct Aid kwa kazi ngumu wanao ifanya ya kusaidia jamii kupitia miradi yake mbali mbali ambayo imeweza kuisadia jamii kwa kila hali.

Kuhusu uzinduzi wa mradi huo amesema Shirika Hilo si linasaidia jamii tu bali limetimiza azma ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kwa vitendo kusaidiana na serikali za mkoa na Wilaya.

“Maji ni uhai tupo unaposaidia watu kutoa maji maana yake unasaidia uhai wa mtu na mimea kwa ujumla” alisema Ayubu Muhamedi.

Kwa upande mwengine Mkuu wa Mkoa huyo amemshukuru balozi wa Kuwait ndugu Jasim Najim kwa kuisadia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kufadhili miradi mbali mbali ya kijamii kama vile maji na elimu.

Aidha kwa upande wa Mkuregenzi wa Shirika Hilo la Direct Aid ndugu Aiman Kamal Din amesema wamejipanga kusaidia sekta ya Elimu Zanzibar kwa kuchimba visima vingi vya maji kwa kila skuli katika maeneo mengi ya manispaa ya mji wa Zanzibar.

Aidha ameitaka Serikali ya Mapinduzi kuendelea kuliunga mkono Shirika hilo kwa kazi zake nyingi kusaidia jamii ili kupunguza gharama za maisha ndogo ndogo kwa jamii ya Zanzibar.

Kwa upande mratibu wa mradi huo mkubwa wa maji kwa Wilaya ya hiyo ya Mjini eneo la Mwanakwerekwe Diwani wa wadi ya Melli nne Salehe Juma Kinana amesema mradi huo umetumia zaidi ya Tsh million Hamsini ili na jumla ya visima vnne vikubwa tayari vimeshafunguliwa.

Kwa upande wake Mwalimu wa Skuli ya Mwanakwerekwe E Rehema Juma akisoma risala ya kwa niaba ya Skuli zote zilizofaidika na mradi huo amelipongeza Shirika La Direct Aid kwa kutumiza ahadi yao waliotoa miezi mitatu nyuma kwa kuwachimbia visima vikubwa vya maji katika eneola skuli zao.

Mradi huo mkubwa huo maji unatarajiwa kufaidisha jumla ya Skuli Tano na majirani wa eneo hilo ikiwemo Ofisi ya mkuu wa wilaya pia mradi huo umefanyika eneo la Magogoni, Sogea , Meli tano na Mwanakwerekwe.

Mkuregenzi wa Direct AID Aiman Kamal Din na baadhi ya wafanya kazi wa shirika hilo akimpokea mkuu wa Mkoa wa Mjini.

 

Mratibu wa Mradi huo wa maji eneo la Kwerekwe Diwani Salehe Juma Kinana akizugumza katika Sherehe hizo za kufungua mradi huo.

 


Mkuu wa mkoa wa Mjini akifungua mradi huo wa maji katika eneo la Mwanakwerekwe .