Kocha Ruvu Shooting akiri ligi Kuu Tanzania Bara ngumu

Kocha mkuu wa klabu ya Ruvu Shoting Abduli Haji Kiduu amesema ligi kuu ya Soka Tanzania bara inautofauti mkubwa na ligi kuu ya Zanzibar, Ligi kuu  ya Tanzania bara ni ngumu zaidi.

Akizugumza  na mtandao huu hapa visiwani Zanzibar kwenye mapumziko baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Tanzania bara, Abduli Kiduu amesema ugumu wa ligi kuu ya Tanzania bara kwa kuwa timu zote huwa makambini na kufanya mandalizi kuwa makubwa ya ligi, udhamini pia ni jambo ambalo linafanya kuwa ligi ya ushindani .

Aidha Kiduu amesema jambo ambalo limefanya timu yake kutofanya vizuri hususani katika hatua za mwanzo dhidi ya Simba ni kupewa timu hiyo akiwa mgeni wa ligi kuu hiyo ya Tanzania bara.

“Mimi peke yangu Ruvu Shoting ndo sijafungwa mechi hata moja uwanja nyumabani mabatini timu zote zimefungwa” alisema kiduu .

Kwa upande wa wachezaji wa Zanzibar ambao husajiliwa ligi kuu ya Tanzania bara kocha kiduu amesema wachezaji hao hupata tabu mwanzo kwa kuwa ligi kuu ya Tanzania bara wachezaji wake wengi ni Fitness mwisho huzoea na kuonekana mali sana.

“Mchezaji yeyote anaetoka ligi kuu ya Zanzibar anaweza kucheza ligi kuu ya Tanzania bara kwa muda mfupi kama atapewa nafasi atakuwa mchezaji mzuri” alisema Kiduu.

Amesema anajivunia Zanzibar kuna makocha wazuri wa mpira wa miguu kutokana na visiwa hivi kupendwa sana mpira wa miguu kuliko michezo mengine.

Abduli Haji Kiduu aliwahi kuwa kocha wa klabu ya Kijichi alipandisha ligi kuu ya Zanzibar na baadae kufundisha klabu ya Jamuhuri Pemba nyumabani kwao alikozaliwa baada ya kumalizika Mashindano ya Mapinduzi Cup mwaka 2016 kajiunga na klabu ya Ruvu Shoting inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara huku akiibakisha kwenye ligi kuu hiyo wakiwa nafasi ya 8.