Vijana watakiwa kuepuka vishawishi vinavyoweza kuwaingiza katika vitendo viovu

Daktari dhamana wa wilaya ya chake chake Mohd Ali jape amesema vijana wanakila sababu za kujiepusha na vishawishi vitakavyo wasababishia kujiingiza katika vitendo viovu.

Akifungua mafunzo ya siku mbili kwa vijana walio naumri chini ya miaka 20 wanaoishi kwenye mazingira magumu huko katika ukumbi wa ofisi ya baraza la mji chake chake amesema kuna vishawishi vingi mitaani hivyo ipo haja kuweza kuviepuka.

Amefahamisha kuwa vijana ndio nguvu kazi ya familia nahata kwa taifa kwa ujumla katika harakati mali mbali nivyema kuweza kujitambua na kuwaelimisha na wengine juu ya maradhi mbali mbali amabayo yatawasababishia kuvunjika kwa ndoto zao zabaadae.

 Aidha amewataka vijanao kujiona kuwa wanabahati maana mazingira wanayoishi nimeema na sio nakama kama wanavyo fkiria watu wengine.

Awala akitoa muongozo kwa washiriki  Afisa Miradi wa SOS Pemba Makame Mtwana Haji amewataka vijana hao kuweza kuyatumia ipasavyo mafunzo watakayo yapata ili yaweze kuwasaidia wengine kwamaslaha yamaisha yao.

Akiwasilisha mada ya Ujana na kujitambua Mwalimu kijana rika kutoka mbizini Pemba Yahya Ali Rashi amesema nilazima vijana wabadilike ili kuweza kutimiza malengo walio jiwekea na kuachana nayale yote ambayo yataweza kukatisha ndoto zao.

Kwaupande wake Rashid Bakar Hamad kijana kutoka shehia ya Tumbe Magharibi amesema watakuwa walimu wazuri pindi watakapo rudi majumbani kwao juu ya Afya ya uzazi kwa vijana ili waweze kuaifahamu ipasavyo.

Mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana wanaoishi mazingira magumu juu ya Afya ya uzazi kwa vijana yameandaliwa na shirika la SOS Pemba na kuwafikia washiriki wa shehia nne Kisiwani Pemba.