Chama cha Madaktari wa michezo kuanzishwa Zanzibar

Daktari  mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar ( Zanzibar Heros) Said Muhamed  amewataka madaktari wenziwe kujitolea kuwasaidia wanamichezo ili kuendeleza michezo .

Akizungumza na zanzibar 24  huko ofisini kwake Zahanati ya makao makuu ya  Polisi Ziwani amesema makocha wanaofundisha timu za vijana hususan watoto wanatakiwa kuwa na utaalamu wa Afya za watoto na aina ya mazoezi sio kila mazoezi wanapangiwa.

Aidha Dk.Said Muhamed amesema Afya ya mchezaji muhimu kwani timu zimekosa kujua misingi ya wachezaji ili kutumiza malengo yao Afya ni sehemu ya malengo hayo alisema Dk Said Muhamed.

Kuhusu majereha kwa wachezaji wengi hususan madaraja ya chini hushindwa kufahamu namna ya kujilinda na kutunza majereha yao amesema baadhi ya wachezaji wamekuwa na mtindo wa kutumia dawa kila wakati wanapo pata majeraha kinyume na taratibu za Afya kitaalam.

“Wachezaji wetu wanapo pata majeraha wanatakiwa wapate muda kupunzika, mazoezi madogo madogo sio kuchoma shindano na dawa kila wakati ‘” Alifahamisha Dk Muhamed.

Kuhusu ulaji na lishe za wachezaji amesema wachezaji wanao cheza ligi wanatakiwa wawe makambini ili kupata ratiba nzuri ya chakula na malazi kwa ujumla na mfumo mzima wa kukaa kambi wa kitaalamu.

“Wachezaji wanatakiwa wanywe maji mengi kila wakati , matunda, mboga mboga na vyakula vyenye majimaji na kuepuka kula ovyo kila aina ya chakula huweza ndio sababu ya kupata maradhi” alisema Dk Muhamed Said.

Kwa upande mwengine Dk Said Muhamed amesema timu nyingi za Zanzibar zimekuwa na wakufunzi wasio na taaluma ya udaktari na hiyo kusababisha majeraha ya siyo na maana.

Mwisho ameelezea wako katika mpango kuanzisha chama cha madaktari wa michezo Zanzibar ili kuinua sekta ya Afya katika michezo.