Miaka 6 ya Uongozi wa Rais Ravia ndani ya ZFA

Hali sio shwari katika visiwa vya Zanzibar kwenye upande wa Soka baada ya vigogo wakubwa waliopewa dhamana ya kuingoza ZFA kujiuzulu wenyewe kwa kuwa wameshindwa kuendesha mpira wa Zanzibar kwa utaalamu na ukweli.

Kwa muda mrefu sana wamekuwa  wakionyesheana vidole wadau wa soka na viongozi wa Chama cha Mpira miguu Zanzibar ( ZFA)  kwa kushindwa kuwa waaminifu katika kuliendeleza Soka la Visiwani.

Leo tumefika hapa tulipofika kwa utashi wetu na malumbano yetu tunakuwa wamoja kwa muda mfupi baadae tunatengana, katika uchambuzi huu tutaangalia japo kwa ufupi miaka sita ya Uongozi wa ZFA chini ya Raisi Ravia Idarous Faina .

Tangu alipopokea kofia ya uongozi kutoka kwa Amani Makungu mwaka 2013 alifanya mengi mazuri yanayohitaji kupongezwa kiasi licha ya kuvuruga mengi, matukio mbali mbali yanahitaji kukumbukwa kwenye utawala wake na kujifunza mengi kutokana na matukio hayo.

KUPEWA UWANACHAMA WA CAF  

Hili ni tukio kubwa sana wakati uongozi wa ndugu Ravia baada ya Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania TFF kupeleka ombi maalum la Zanzibar kuwa mwanachama kamili wa CAF jambo ambalo Raisi Ravia lingempa sifa kubwa kama lingetimia bila ya  utata.

Nchi 53 kuipa kura Zanzibar kuwa mwanachama wa CAF bila ya pingamizi na udogo wa nchi yake bila ya kufanya kampeni yoyote ambayo wajumbe waliridhia kwa tafsiri ya mpira Zanzibar inakubalika kama nchi inayo weza kujiendesha kisoka bila ya kutegemea upande wa pili wa Muungano.

Ni jambo la Faraja kwa Zanzibar licha ya kupoteza uwanachama huo ila tarehe 16 mwezi machi mwaka 2017 Ravia na Uongozi wake watakumbukwa kwa hili si yeye tu hata aliyekuwa Raisi wa TFF Jamal Malinzi na aliyekuwa Raisi wa CAF Issa Hayotou watakumbukwa kwa hili.

UKIMYA BAADA YA KUONDOLEWA CAF 

Tarehe 14 mwezi wa saba mwaka 2017 itabaki kuwa ni gumzo na mihemko ya Zanzibar kundolewa CAF kwa kigezo cha kanuni ziliachwa kuwa Zanzibar hana sifa ya kuwa mwanachama kamili wa CAF.

Tulitegemea sana kuona viongozi wakubwa ndani ya ZFA wanalikingia kifua jambo hili na kutoa muongozo kwa wadau na wananchi kwa kitendo kile kimeidhalilisha Zanzibar Duniani kote ni sawa na kuoa na kupokonywa mke, tulitegemea maneno mazuri kutoka kwake lakini haikua hivyo.

Ravia Idarous Faina yeye mwenyewe ndie aliepokea kijiti cha uwanachama na yeye ndie alipokea barua ya kuondoshwa lakini hakuna kilicho fanyika baada ya kuondolewa zaidi ya kubaki story.

KESI MAHAKAMANI NA KUSIMAMA KWA LIGI

Huu haukuwa mwaka mzuri kwa soka la Zanzibar na kutia doa soka la Zanzibar kwa muda sana licha ya tukio lile lilifanya kuonekana ZFA ipo kimigogoro na si kwa kundesha mpira wa Zanzibar.

Hi ilikuwa mwaka 2015 baada ya aliyekuwa Makamo wa Rais wa ZFA Unguja Haji Amer Mpakia kufungua mashtaka dhdi ya Rais Ravia na Makamo wa Rais Pemba Ali Muhamed kwa ubadhirifu wa fedha jambo lililofanya msimu huo kuzorota kwa ligi hadi pale Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein kuingilia suala hilo.

Tarehe 22 April 2017 ndipo Chama hicho na kamati tendaji chini ya Baraza la Michezo Zanzibar kumfungia miaka 4 kutojihusisha na masuala ya mpira Makamo Rais huyo wa ZFA Haji Ameri Mpakia.

KUCHEZA LIGI KUU NA HAKUNA TIMU ILOSHUKA

Ni miongoni mwa mambo ambayo hayata sahauliwa kwenye miaka 6 ya ungozi wa ZFA chini ya Rais Ravia licha ya  msimu mwaka 2015/2016 wa ligi kuu ya Zanzibar kuwa na timu nyingi lakini hazikushuka daraja bali zilipanda nne daraja kwa kanda zote Unguja na Pemba.

Jambo ambalo limekemewa na wadau wa soka wa Zanzibar licha ya vilabu kutia ulimi puani kwenye jambo hili na kuona linafaida kwao ila uongozi wa ZFA haukuwa imara kushindwa kusimamia kanuni ya ligi ya Zanzibar na kubadilika bila sababu jumla ya timu 36 kwa kanda zote zilicheza msimu wa mwaka 2016 kwa kuwa hakuna kushuka daraja .

SOKA LA UFEKWENI KUPATA UMARUFU      

Wakati wa utawala wa Rais Ravia na ungozi wake ulipata mafaniko  makubwa baada ya Zanzibar kushinda katika Mashindano ya COPA DAR ES SALAAM BEACH SOCCER  yaliyofanyika kwenye fukwe za COCO BEACH na kuifanya zanzibar kuwa wababe wa soka la ufukweni licha ya changamoto mbalimbali.

Hayo yamefanywa chini ya Uongozi wa Raisi Ravia kama Raisi wa chama hicho ni mema na mazuri pale alipoahidi kwa mdomo wake kutenga fedha za kwaa jili ya soka la Wanawake na Ufukweni jambo ambalo lingesaidia kukuza michezo katika uongozi wake wote ndugu Ravia.

MIAKA MITATU YA UDHAMINI WA GRAND MALT

Alipopokea kijiti cha ungozi kutoka kwa Amani Makungu Rais Ravia alifanya mambo mengi makubwa kukuza mpira ngazi ya vilabu na kuleta neema kwa timu za Zanzibar na kufungua soka kwa timu zilizotoka mashamba  kama vile Mtende Rangers kuonyesha ushindani wa kweli.

Kipindi hicho sio sana kuona ligi kuu ya Zanzibar inakuwa na mipango mibovu na kuona Bingwa anavyopatikana na hakukuwa na mfumo wa kucheza kanda yaani Unguja na Pemba na kufanya mpira kutoka kisiwa cha Pemba kukuwa kwa kasi sana.

ZANZIBAR HEROS KUFANYA MAKUBWA KENYA

Hakuna asiejua Zanzibar Heroes ilifanya nini kule Kenya na kuwa gumzo mitaani licha ya kuonekana wachezaji ndio bidii yao na kocha Moroko, hapana uongozi wa Ravia ulijitahidi kushughulika na timu ile tangu maandalizi ya awali ya safari kabla yale ya mwisho ambayo yalikuwa ya shangwe sana.

Lazima tujivinie kwa hili kwani Ravia alisimama kama Rais wa ZFA na kuweza kuleta taswira mpya kwa mpira wa Zanzibar na kuonekana vijana wa Zanzibar wanaweza kama watapewa nafasi ya kushiriki Mashindano ya kimataifa .

Kuchukua nafasi ya pili kwenye michuano ya CECAFA CHALLENGE CUP sio jambo la kawaida na aina ya mpira ulionyeshwa ni wazi kwamba Uongozi wa Ravia pamoja na mapungufu yao  ila walifanya la maana na tutaendelea kuwakumbuka.

Yako mengi walifanya mazuri na mabaya ila wao ni Binadamu licha ya mapungufu yao binafsi hatuwezi kuyajadili yote, tunahitajika kuwapa hongera kwa kile walichokifanya katika miaka 6 ya uongozi wao.

Tujifunze kila binadamu ana mapungufu yake lakini siyo sababu ya kuvuruga utawala kwa jambo fulani. Sasa kazi kubwa kwa wale watakao taka kuongoza mpira wa Zanzibar kwa kipindi kinacho endelea kama watatumia makosa yalopita ni kuwa ni funzo basi tutafika mbali kwenye soka la Zanzibar kwa ujumla .

MUNGU AMETUBARIKIA UNGUJA NA PEMBA YOTE.